Friday 26 April 2013

FONOLOJIA YA KISWAHILI NI PANA JADILI

I. UTANGULIZI: Maana ya Fonolojia Asili ya neno Fonolojia Aina za mofolojia II. KIINI: • Vipengele vya Fonolojia • Chimbuko la Fonolojia • Historia ya fonolojia • Mahusiano kati ya Fonolojia na tanzu nyingine za isimu ambazo ni;  Mofolojia  Semantikia  Sintaksia III. HITIMISHO IV. MAREJEREO. Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika mfumo fulani. (TUKI, 1990). Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi,uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha ya binadamu.(Massamba na wenzake, 2004:6) Fonolojia ni mtaala wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani na uamilifu wao ndani ya lugha husika.(Hartman, 1972). Fonolojia ni kiwango mojawapo cha lugha fulani kilicho na vipashio vidogo zaidi kuliko vipashio vingine vyote vya lugha, vipashio hivyo ni fonimu na alofoni zake.(Fudge, 1973). Fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia hushughulikia jinsi sauti hizi zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana.(Habwe na kalanje, 2004). Kwa ujumla Fonolojia ni taaluma ya isimu ya lugha inayoshughulikia sauti za lugha husika kwa kuchunguza mahusiano na maathiriano ya sauti hizo. Kietimolojia, neno Fonolojia limetokana na maneno mawili ya Kigiriki ambayo ni foni au phone na logos. Foni likiwa na maana ya sauti au uneni na logos inamaanisha stadi au taaluma ya lugha mahususi. Taaluma hii inajikita katika kushughulikia hasa sauti zile ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi. Fonolojia imegawanywa katika aina kuu mbili ambazo ni Fonolojia arudhi na vipande sauti. Fonolojia vipande sauti ni aina ya Fonolojia ambayo hushughulikia uchunguzi wa vipande sauti vyenyewe. Wanaisimu katika aina hii ubainisha vipande sauti bainifu katika lugha kama vile alofoni na fonimu pia kueleza fonimu hizo jinsi zinavyoweza kuathiriana katika maeneo mbalimbali. (Mgullu, 2010). Aina nyingine ya Fonolojia ni Fonolojia arudhi ambayo kwayo hushughulikia masuala mengine ya sauti ambayo haiathiri vipashio vikubwa zaidi kuliko fonimu moja. Pia aina hii uchunguza mfumo wa kuweka mkazo katika maneno na tungokatika lugha fulani kama vile kiimbo na muundo wa silabi. (Mgullu, 2010). Fonolojia ya Kiswahili hujishughulisha na vipengele mbalimbali ambavyo vinahusiana na sauti pamoja na mpangilio wake wa uundaji maneno katika lugha mbalimbali. Vipengele ni kama vile; matamshi,kiimbo, mkazo, na mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu na mfuatano wa mofimo katika kuunda maneno na mengineyo. Silabi ni kipashio cha utamkaji ambacho kwa kawaida ni kikubwa kuliko fonimu na kidogo kuliko neno. Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ya sauti za lugha zinatamkwa kwa pamoja kama fungu moja linalojitegemea kimatamshi. Fungu hilo laweza kujumuhisha sauti moja pekee au sauti mbili kutegemea muundo wa lugha husika. (Massamba na wenzake, 2004). Mpaka wa silabi hutenganishwa na alama ifuatayo; $ mfano: $ma$$ma$, $a$$na$$ku$$la$. Kiimbo ni utaratibu maalumu wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika usemaji wa lugha au kiimbo ni kipengele cha Fonolojia chenye maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti za lugha. Vilvile kiimbo ndicho kinafanya sentensi iwe ya swali,mshangao mkebei au maelezo. Mfano. John ameondoka? John ameondoka. John ameondoka.

No comments:

Post a Comment

soma na uelewe