FASIHI YA AFRIKA
DONDOO
1. UTANGULIZI
-
Fasili ya dhana za msingi
-
Mjadala kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa Thieta ya jadi ya
Kiswahili
2. MADA
-
Thieta ya jadi ya Kiswahili ni nini/ipi
-
Sifa za Thieta ya jadi ya Kiswahili/Kiafrika
3. HITIMISHO
Makala hii inakusudia kubainisha
sifa za thieta ya jadi ya Kiswahili /Kiafrika,lakini kabla ya kujikita katika
mada yenyewe, dhana za msingi zitafafanuliwa kwanza ili kumwezesha msomaji
kuelewa akutanapo na dhana hizo katika makala hii. Dhana hizo ni pamoja na
miviga, drama/tamthiliya na sanaa za maonesho/thieta.
Kerr(1995:1) anasema; Drama refers to displays of actions to
an audience, in which there is an imitation of events in the real or supernatural world and there is an
element of story or suspence.
Kwamba, Drama ni kuonesha matendo kwa hadhira,ambapo kuna kuiga matukio
halisi au matukio ya kimiujiza na kuna elementi ya hadithi au taharuki.
(Tafsiri yetu)
Ni matendo yanayoletwa mbele ya hadhira na ndani mwake kuna kuiga
matukio katika hali halisi au ya kidhahania.
Kerr(1995:1) akifasili miviga
anasema; Ritual refers to an action which is undertaken to
give homage to,obtain assistance from,or in some way intercede with
supernatural forces. This may or may not involve dramatic representation.
Kuwa, ni kitendo kinachofanyika kwa lengo la kutoa heshima, kupata
msaada,au kwa namna fulani kuomba nguvu za kimiungu. Hii inaweza kuhusisha au
isihusishe uigizaji (Tafsiri yetu)
Naye Wamitila (2003:128) katika Kamusi ya Fasihi,Istilahi na Nadharia
anasema Miviga ni dhana inayotumika
kuelezea sherehe ambazo aghalabu hufanywa katika kipindi maalumu katika jamii
fulani. Aghalabu sherehe hizi hufanywa kwa sababu mbalimbali,kwa mfano, huweza
kufanywa ili kumtoa mtu kutoka kundi moja la kijamii hadi jingine.
Sanaa za maonyesho zinajumuisha zile sanaa ambazo huwasilisha
,ana kwa ana, wazo kwa hadhira kwa kutumia usanii wa kiutendaji. Mlama
(1983:186)
Pia anasema ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo,mchezaji, uwanja
wa kuchezea na watazamaji.
Kerr (1995:1) anasema; Theatre cover drama, many forms of ritual, dance,and other perfoming arts
such as acrobatics,mime and semi dramatized narratives.
Thieta hujumuisha drama,miviga,dansi,na sanaa nyinginezo za vitendo
kama vile sarakasi,uigizaji bubu na simulizi za kidrama( Tafsiri yetu)
Mabweazara (uk 11) naye anasema,
Theatre can be defined as an activity in which an actor takes a role other than
himself and through mime, speech, song and dance movements conveys or
communicates a message to an audience, this is an aspect that has always been
deeply ingrained in African life styles.(kutoka tovuti)
Thieta inaweza kufasiliwa kama kazi ambapo mwigizaji anachukua uhusika
zaidi ya yeye mwenyewe kupitia uigizaji bubu, maneno, nyimbo na miondoko ya
kimuziki kuwasilisha ujumbe kwa hadhira. Kipengele hiki kinafungamana na mtindo
wa maisha ya Mwafrika.(Tafsiri yetu)
Pamoja na kwamba wataalamu mbalimbali hutumia dhana ya drama na
tamthiliya kumaanisha kitu kilekile,tunaweza kusema kuwa kuna utofauti kwa kiasi
fulani ambapo usanii wa kiutendaji
katika drama hutegemea zaidi vitendo na uongeaji tofauti na ilivyo katika
tamthiliya ambayo inakuwa imeandikwa kwa lengo la kuoneshwa kwa hadhira.
MJADALA KUHUSU KUWEPO AU KUTOKUWEPO KWA THIETA YA JADI YA KISWAHILI/KIAFRIKA
Kuna mitazamo miwili kuhusu uwepo wa thieta ya jadi ya
Kiswahili/Kiafrika
I. Mtazamo wa Kimagharibi (Eurocentric view)
Ii. Mtazamo wa Kiafrika
(Afrocentric view)
I.
Mtazamo wa Kimagharibi
Mtazamo huu unawahusu wanazuoni mbalimbali, baadhi yao ni Ruth Finegan,
Adande, Dadi na Burton. Wao wanasema Afrika haikuwa na kitu kinachoitwa sanaa
za maonesho kama Ulaya, kwani sanaa hizo zilihusisha sehemu maalumu ya
kuoneshea(ukumbi), ulipaji wa kiingilio kwa hadhira, fanani kulipwa, mazoezi kwa
ajili ya maonesho na matangazo mbalimbali katika vyombo vya habari kama redio,
runinga, na magazeti/majarida.
Hata hivyo wanasema kama ilikuwepo basi ni kidogo sana, au la iilikuwa
katika hatua changa sana (tete). Finegan(1970:500) anasema; It would perhaps be true to say that in
Africa,in contrast to Western Europe and Asia, drama is not typically a
wide-spread or a developed form.
Katika mjadala wa Lo Lyong mwaka 1975 kuhusu sanaa za maonyesho za jadi
anasema hakuna kitu kigeni kiutamaduni
Afrika kama wazo la sanaa za maonesho. Anaendelea kusema kuwa Uli Beier,
ambaye anajua zaidi kuhusu utamaduni wa Wayoruba kuliko Myoruba yeyote anasema
wazi kuwa hakuna sanaa za maonesho zilizojisimika katika mila na desturi za
Wayoruba.
Wanazuoni hao na wengine wenye mawazo hayo ni wale wanaochambua
utamaduni wa Mwafrika bila ya kuhusisha na utaratibu mzima wa kuzalisha
mahitaji muhimu ya maisha. Ikiwa Mwafrika siku zote amekuwa akijishughulisha
katika harakati hizi, vipi tuseme hakuwa na sanaa zake? (Bakari 1995: 3)
II.
Mtazamo wa Kiafrika
Unahusisha wanazuoni mbalimbali, baadhi yao ni Penina Mlama, Leshoai,
Kerr, Lihamba,Mukotani Rugyendo na Ebrahim Hussein. Wao wanathibitisha uwepo wa
sanaa za maonesho kwa kutumia ushahidi wa majigambo unaopatikana katika ukanda
wa ziwa mfano Bahima na Bahaya, miviga, ngoma na utambaji hadithi nk.
Mlama (1991:56) anatoa mfano wa majigambo toka Bahaya kama ifuatavyo;
I am a tough
character
My soul is
likened to a tobacco leaf
My heart to a wooden spoon
Which of the
two is better
It is you my
lord the king who worries my mind
I am totaly
commited to defending the kingdom
Kwa ujumla wataalamu hawa wenye mtazamo wa Kiafrika wanasema sanaa za
maonesho ni dhana inayojitegemea bila ya kulinganishwa na kitu chochote kutoka
nje, Hivyo ni zao la jamii husika.
CHANZO CHA MJADALA HUO
Chanzo cha mjadala huo
kilitokana na nadharia ya ulinganishi (comparative approach) iliyolinganisha
vitu kwa kuzingatia chimbuko, athari na raghba(interest) na pia tatizo hili
limetokana na kutumika kwa lugha ya Kiingereza katika kufafanua dhana za thieta
ya jadi. Ili kuweza kutatua mgogoro huu sharti kwanza wanazuoni wa Kiafrika
wajadiliane na wafanye utafiti juu ya istilahi muafaka zitakazotumika kufafanua
sanaa za maonyesho za Afrika.
Ricard(2000:14) anasema; A debate on the existence of theatre in
Africa was raging in the West. Kwamba mjadala
kuhusu uwepo wa thieta Afrika ulianzia kwenye nchi za kimagharibi( tafsiri
yetu)
Hivyo basi,kwa hoja hizo, sisi kama wanakikundi tunaungana na mtazamo
wa Kiafrika kwamba thieta ya jadi ya Kiswahili ilikuwepo. Katika kufanya
hivyo,tutabainisha sifa za thieta ya jadi ya Kiswahili, jambo ambalo makala hii
inakusudia kushughulikia.
Ikumbukwe kwamba Sanaa za maonesho katika Tanzania ya leo ziko za aina
mbili, yaani sanaa za maonesho ya jadi na sanaa za maonesho mamboleo. Sanaa za
maonesho ya jadi ya Kiswahili ni zile ambazo zina chanzo na msingi katika jamii
ya Tanzania. Sanaa hizi ni pamoja na ngoma, majigambo, sherehe za jando na
unyago,matambiko na ngomezi. Katika shughuli hizi watu hufanya vitendo vya
kisanaa kama vile uchezaji ngoma, uimbaji,upigaji muziki, utongoaji
mashairi,vikiambatana na matendo ya mwili na matumizi ya lugha.
Vitendo hivi vya kisanaa ni njia mojawapo bora ya kuwasiliana kati ya
watu na watu wengine au miungu na mizimu katika jitihada za kuyakabili mazingira
na kuendeleza jamii. Kwa kucheza ngoma watoto hufunzwa tabia inayotegemewa
katika utu uzima, kwa kuimba miungu huelezwa matatizo ya ukame,magonjwa nk, kwa
kusimulia hadithi watu hufunzwa historia ya jamii ,tabia nzuri,jinsi ya kuishi
na watu wengine, kwa kuimba na kufanya vitendo vya kuigiza wenye tabia mbaya
hukosolewa na kurekebishwa .
Hatar A.(2001:4) akimnukuu Mlama(1983)
anasema ; We are using theatre not
in the Western Classical tradition of stage, perfomers and an audience, but in
the more general form of “symbolic perfomance, with symbolic images
representing life through action”. Such symbolic perfomance could include
dance,storytelling,poetic recitations, some rituals, dramatizations and so on.
Hatutumii thieta kwa misingi ya Kimagharibi ya kuwepo kwa
jukwaa,watendaji na hadhira bali kwa namna ya kijumla zaidi ya kutumia
watendaji kiishara kwa picha za kiishara kuwakilisha hali halisi ya maisha
kivitendo. Utendaji huo unaweza kujumuisha dansi,utambaji hadithi,miviga,drama
nakadhalika.( tafsiri yetu)
Semzaba(1973:5) anasema; sanaa za maonesho za jadi ni zile sanaa
ambazo hazijaathiriwa wala kuingiliwa kwa mtindo wowote na namna yoyote.
(Tafsiri yetu)
Kwa upande mwingine, sanaa za maonesho mamboleo ni zile zinazotokana na
athari za ustaarabu wa kigeni hususan
tamthiliya ambayo ililetwa kwetu na Waingereza wakati wa ukoloni, awali kwa
lengo la kujifurahisha na kujikumbusha maisha ya kwao. Mlama (1976:38) Si lengo la makala hii kujadili aina hii ya
sanaa za maonyesho. Lengo hapa ni kujadili sifa za thieta ya kijadi ya Kiswahili/Kiafrika.
Sanaa za maonesho za jadi zilifungamana na kazi za kila siku za jamii
husika. Mabweazara(uk 11) anasema; indigenous African theatre was deeply rooted
in day-to-day activities. It was part and parcel of the whole conception of
existence,and it was also a communal activity. It existed within its functional
context, and it sought to perpetuate the virtues of society and purge all
evil.
Naye Semzaba (1973:5) anasema; Thieta ya jadi ya Kiswahili ilifungamana
na mifumo iliyoimarika vya kutosha au
uumbaji wa sanaa ulio imara katika jamii, na uwepo wa utamaduni au tamaduni kwa
maendeleo ya mifumo hii katika makundi hayo ya kijamii.(Tafsiri yetu)
Sanaa za maonyesho za jadi zilikuwa na sifa ya kuonekana kimatendo.
Mlama (1976: 188) anasema kwa bahati mbaya sanaa za maonyesho za jadi zilipigwa
vita zaidi ya vipengele vingine vya utamaduni wa wenyeji hasa kwa sababu sanaa
hizi zilionekana kimatendo.
Pia sanaa za maonesho za jadi
zilijisimika katika utamaduni, mila na desturi za jamii husika.
Mlama(1976:190). Kama tulivyoona kuwa thieta ya jadi ya Kiswahili inafungamana
na kazi za kila siku na maisha kwa ujumla, ni wazi kabisa kwamba ni vigumu
mila,desturi na utamaduni wa jamii husika kuepukika katika thieta ya jamii hiyo.
Pre-colonial Tanzania’s theatres
therefore were part and parcel of the people’s way of life, and the perfomances
were in direct responce to the people’s interpretation of meaningful phenomena.
Kwa hiyo sanaa za maonesho za anzania kabla ya ukoloni zilikuwa ni
sehemu ya maisha ya watu, na matendo yalikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya
tafsiri ya watu juu ya matukio ya kweli katika maisha(Tafsiri yetu)
Vilevile Mlama 1983:4 anasema Pre-colonial African theatre was
essentially utilitarian and sought to raise,discuss and impart societal norms,
as well as be able to them on to successors generations. This was not art for
arts sake, but art for specific,or as we would now say, specific purposes.
Kimsingi sanaa za maonesho za jadi zilikuwa na lengo maalumu lililokusudiwa kuibua, kujadili na
kuathiri mila za kijamii na kuweza kuzirithisha kwenye vizazi vinavyofuata. Hii
haikuwa sanaa kama sanaa tu, bali sanaa kwa kusudi maalumu.(Tafsiri yetu)
Pia anasema kuwa utendaji katika
sanaa hizo ulikuwa shirikishi,and often the audience merged with the
performers, and anyone with a spark of inspiraion cold pick up the song
wherever.
Naye Kerr (1995:2) anasema
kuwa: the notion of a
communal,sharing,pre-colonial society has found a theatrical equivalent in an
aesthetics emphasis on African theatre’s anonymous,participatory qualities in
contrast with divisive individualism of colonial Western theatre. Mbweazara (uk
12) anasema unlike in the Western forms of theatre, the audience in the Chiware
ceremony is part of the entire activity-it does not watch from without but
participates actively in the entire ceremony.
Vilevile thieta ya jadi ya Kiswahili ilikuwa mali ya jamii nzima. Hii
ni kutokana na kwamba ilichukuliwa kama sehemu ya kazi za kila siku.
Kerr (1995:5) anawasisitiza wanathieta wa kiafrika kugeuka na kutumia
mbinu ya thieta ya jadi ya collectivity’socialism’. Anasema;
There are clear homologies
here with political theories urging a return to pre-colonial communocratic
values.
Pia tamthiliya za jadi za Kiswahili ziliendana na ngoma na miviga.
Ngoma ni pamoja na sherehe, utawala na taratibu nzima. Ngoma inahusishwa na
nguvu fulani ambapo nguvu hiyo ina imani fulani.
Thieta za jadi ya Kiswahili
ilifungamana na dini za kijadi, mizimu na miungu. Matambiko mbalimbali
yalifanyika kwa lengo la kuiomba miungu mambo mbalimbali kama vile mvua na
kujiepusha na balaa na magonjwa mbalimbali. Hii inafungamana moja kwa moja na
ontolojia ya Kiafrika.
Vilevile thieta ya jadi ya Kiswahili ilifungamana na muktadha kutegemea
na na shughuli nzima ya wakati huo,hakukuwa na ukumbi maalum wa kwa ajili ya
sanaa za maonesho . kwa mfano, ngoma ilichezwa kulingana na kusudi la wakati
huo na mahali ambapo ngoma hiyo inakusudiwa ktoa funzo fulani wakati huo kwa
hadhira fulani.
Mulokozi (1996:190) anasema hapa Afrika,
kumbukumbu za kwanza za maigizo ya
kitamthiliya tunazipata Misri,ambako michezo ya miviga iliyohusu kufa na
kufufuka kwa Mungu wa Wamisri aliyeitwa Osiris ilikuwa ikiigizwa kila mwaka.
Anaendelea kusema kuwa mbali na drama za kimisri ambazo huenda
ziliandikwa,maigizo yasiyoandikwa hapa Afrika yalikuwa ni sehemu ya matendo
mengi ya kijamii, hasa katika miviga na ngoma. Halikadhalika ,tamthiliya
bubu(mime), maigizo ya watoto na maigizo ya watani yalikuwepo tangu zamani.
Mulokozi anasema kuwa hata hivyo drama hizi zilifungamana na fasihi simulizi,
hazikuwa za kibiashara, hazikurasmishwa na hazikuandikwa. Tamthiliya
zilizoandikwa ili ziigizwe rasmi jukwaani ni matokeo ya athari ya tamthiliya za
Ulaya.
Katika kipengele cha kurasimishwa, tunaona kwamba kuna utata kwa sababu
kila jamii ilikuwa na fani maalumu zilizotumika katika jamii hiyo kwa lengo
maalumu. Kwa mfano jamii ya Wahaya ilikuwa na majigambo ya ushujaa.
Mulokozi (1996:211) akijadili suala la thieta ya umma, anasema kuwa
mbinu za sanaa za maonesho za jadi zilitumika, na baadhi ya mbinu hizo ni;
Nyimbo na ngoma, Lugha sadifu kulingana na mazingira, Maudhui yanayoakisi
maisha na matatizo ya watu wenyewe na
yanayoendeleza maslahi yao, Ushirikishwaji wa mtu yeyote badala ya
wataalamu tu katika sanaa na Matumizi ya ishara, maigizo-bubu, na mbinu
nyingine za kijadi.
Kwa ujumla sanaa za maonesho za Kiafrika ni dhana inayotendeka, na ili
dhana hiyo itendeke inahitaji mambo yafuatayo; Dhana inayotendeka mfano ngoma, tambiko,
miviga na nyimbo, Mtendaji –hapa itategemea kinachotendeka mf manju,kungwi na
ngariba, Uwanja wa kutendea hapa inategemea na dhana inayotendeka, kwa kawaida
jukwaa hubadilika badilika , Watazamaji ambapo watazamaji wanaweza kuwa na
nafasi mbili ya utazamaji na yautendaji. Mfano mtazamaji anaweza kushiriki
kuimba wimbo,kucheza na kupiga vigelegele ili kuonesha kilele chake cha furaha.
Vipengele hivi ni kwa mujibu wa Mlama(1981:153). Mulokozi anakubaliana
na vipengele hivyo na kuongeza kipengele
cha ubunifu na kusudio la sanaa hiyo.
Semzaba (1973:5) anasema; Thieta ya jadi ya Kiswahili ilifungamana
na mifumo iliyoimarika vya kutosha au
uumbaji wa sanaa ulio imara katika jamii, na uwepo wa utamaduni au tamaduni kwa
maendeleo ya mifumo hii katika makundi hayo ya kijamii.(Tafsiri yetu)
Hivyo basi, tunaweza kuhitimisha mjadala wetu kwa hoja kwamba, thieta
ya jadi ya Kiswahili ilikuwepo na ilifungamana na kazi za kila siku. Suala la
kutokuwepo kwa sanaa za maonesho Afrika kwa mtazamo wa kimagharibi halina
mashiko kutokana na nadharia ya ulinganishi na dhana walizotumia. Jamii huwa
zinatofautina katika nyanja mbalimbali za maisha, hakuna jamii zinazofanana.
Hivyo tunapendekeza zitumike dhana ambazo zinawakilisha thieta ya Kiswahili/
Kiafrika badala ya kutumia dhana za Kimagharibi, pamoja na kujikita katika
misingi ya thieta ya jadi ya kiswahili ili kuondoa utata uliopo.
MAREJEO
Bakari J. A na
Materego G.R (1995), Sanaa kwa
maendeleo: Stadi, Mbinu na
Mazoezi, Amana Publishers, Dar es salam.
Etherton M.
(1982), The Development of African Drama; Africana Publishing
Company, New
York.
Finnegan R (1970),
Oral literature in Africa;
Oxford University Press, Nairobi.
Hatar A (2001), ‘The state of Theatre Education in Tanzania’,
prepared for
UNESCO,
University of Dar es salaam.
Kerr D (1997) , African Popula Theatre by David Phillip
Publishers(pty) ltd,
Claremont 7735 Cape
Town.
Mlama P (1981) , ‘Sanaa za maonesho katika jamii ya
asili’ katika Omari C.K
Na M.Mvungi; Urithi wa utamaduni wetu, Tanzania
Publishing House,
Dar es salaam
Mlama P. (1991), Culture
and Development; The Popular Theatre Approach,
Uppsala,
Nordiska Afrikainstitutet.
Muhando P. na
Balisidya N.(1976) , Fasihi na Sanaa za Maonesho, Tanzania
Publishing House, Dar es Salaam.
Ricard A.
(2000), Ebrahim Hussein : Swahili Theatre and Individualism na Nyota
Publication, Dar
es Salaam
Semzaba, E.
(1973), Trends in Modern African Theatre movement, M.A Thesis,
University of
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
soma na uelewe